
KASEKENYA- TANROADS NA WANANCHI LINDENI BARABARA
Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kushirikiana na wananchi kulinda hifadhi za barabara na hivyo kuwezesha ujenzi wa miundombinu hiyo kufanyika kwa urahisi na kudumu kwa muda mrefu. Akikagua ujenzi wa barabara ya Mkuranga-Kisiju KM 45 na barabara ya Kilwa mkoani Pwani amehimiza ushirikishwaji wa wananchi…