
Polisi yawaachia kina Mbowe kwa dhamana, baadhi wakwama
Mbeya. Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kuwashikilia na kuwahoji viongozi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wapatao 520 na kuwaachia huru baadhi yao kwa dhamana. Pia limesema ambao hawakuachiwa ni wale walioshindwa kukidhi masharti ya dhamana au kuwa na makosa zaidi ya moja, ikiwemo jinai. Limesema halitasita kuchukua hatua kwa yeyote…