Ni Meridianbet tena ndani ya Kijitonyama

  Meridianbet tena ndani ya Kijitonyama ndivyo unavyoweza kusema kwakua leo tena wamefanikiwa kufika kwenye eneo hilo na kutoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu mbili ambazo zinapatikana maeneo hayo. Huu ni utamaduni ambao wameujenga Meridianbet kwa muda mrefu kuhakikisha wanarudisha kwenye jamii, Hivo leo wameamua kurudisha kwenye jamii kwa kutoa msaada wa vifaa…

Read More

Dk Biteko azindua kituo cha kupokea, kupooza umeme GGML

Geita. Mgodi wa Uchimbaji Madini ya Dhahabu wa Geita (GGML), umeandika historia baada ya  kuanza kutumia umeme wa gridi ya Taifa kwa mara ya kwanza kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupooza umeme. Kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya Dola 25.8 milioni (Sh67.08 bilioni). Mgodi huo ulioanza kufanya kazi mwaka 2000,…

Read More

Mfumko wa bei wapungua, sababu yatajwa

Unguja. Mfumko wa bei kwa kipindi cha miezi 12 hadi kifikia Julai 2024 umepungua na kufikia asilimia 5.26 kutoka asilimia 5.65 iliyorekodiwa kwa kipindi cha Juni mwaka jana, Zanzibar. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Agosti 13, 2024 mtakwimu kutoka divisheni ya takwimu na bei, Hassan Jamal Hassan amesema kundi la bidhaa za chakula na…

Read More

Wataalamu 250 wa afya ulimwenguni kukutana Tanzania

Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kisayansi la Kimataifa la Matumizi ya Mawimbi Sauti katika Tiba (ISMRM) pamoja na Tiba ya Mishipa ya Fahamu (Neuroradiology) litakalofanyika Septemba 19 hadi 20, 2024 jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limeratibiwa nchini na Chama cha Madaktari Bingwa wa Rediolojia Tanzania (Taraso); Chama cha Wataalamu…

Read More

Serikali mbioni kufunga Ziwa Victoria

Mwanza. Ikiwa imebaki siku moja Ziwa Tanganyika lifunguliwe Agosti 15, 2024, Serikali imewataka wasimamizi wa Ziwa Victoria kuandaa mkakati wa kulifunga. Ziwa Tanganyika lilifungwa Mei 15, 2024, ili kutoa nafasi kwa ziwa hilo kupumzika na mazao ya uvuvi kuzaliana na kuongezeka ziwani. Akizungumza leo Jumanne Agosti 13, 2024, kwenye ufunguzi wa kongamano la Ukuzaji viumbe…

Read More

Kilio wizi mita za maji Manispaa ya Iringa

Iringa. Wakazi wa Manispaa ya Iringa wamelalamikia ongezeko la wizi wa mita za maji unaoendelea katika manispaa hiyo, hali inayosababisha hasara kubwa kwa kulazimika kununua mita nyingine kila wakati. Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Agosti 13, 2024, wananchi hao wamesema wizi huo umekuwa ukitokea katika mitaa ya Mawelewele, Kihesa, Mkwawa, Gangilonga na maeneo mengine,…

Read More