Awesu sasa rasmi ni Simba, atua kambini

Muda mchache baada ya kumalizana na KMC kumng’oa kiungo, Awesu Awesu mchezaji huyo tayari ameungana na wenzake kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu  Bara dhidi ya Tabora United Agosti 17. 

Awesu Awesu dili lake na Simba licha ya kutambulishwa halikukamilika na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji iliamuru kiungo huyo kurudi KMC hadi hapo Simba watakapofuata taratibu za kumsajili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na KMC umethibitisha makubaliano ya pande mbili kuuziana kwa mchezaji huyo yamekamilika na sasa ni mali halali ya Simba.

“Makubaliano ya uamisho wa Awesu kwenda Simba yamefikiwa baada ya vikao vya timu zote mbili, tunamtakia kila la kheri mchezaji huyo ambaye amedumu kikosini kwa miaka miwili akiwa nahodha.” Imesema taarifa hiyo ya KMC.

Kiungo huyo ambaye awali alitua Simba baada ya kuvunja mkataba wake na kuilipa timu yake ya zamani KMC Sh. 50 milion alitambulishwa na Simba na kufanya nayo mazoezi ya kujiandaa na msimu alishindwa kucheza mchezo wa Ngao ya Jamii kutokana na kuzuiliwa.

Awesu jana alionekana akiwa na wachezaji wenzake wa Simba lakini jijini Dar es Salaam zikiwa ni saa chache kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Simba itakuwa timu mwenyeji wa Tabora kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa KMC jijini Dar es Salaam 10:30 jioni.

Related Posts