Nablus. Walowezi wa Kiyahudi wamevamia kijiji cha Jit, kilichoko Ukingo wa Magharibi, usiku wa kuamkia Agosti 16, 2024.
Walirusha mawe na mabomu ya petroli, wakachoma moto nyumba na magari.
Wizara ya Afya ya Palestina imeripoti kwamba kijana mmoja wa miaka 20 ameuawa katika shambulio hilo, na mwingine amejeruhiwa kifuani.
Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limesema kuwa linachunguza tukio hilo na limemtia mbaroni raia mmoja wa Israeli.
Viongozi wa Israeli wamekemea shambulio hilo na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wahusika.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu imesema waliohusika na vitendo vya uhalifu watakamatwa na kushtakiwa.
Rais wa Israeli, Isaac Herzog amelaani vitendo vya uhalifu na kutaka hatua zichukuliwe haraka dhidi ya wahusika.
Video zilizopigwa zikionyesha nyumba na magari yakiteketea na moshi mkubwa ukitoka kijijini.
IDF imesema vikosi vyake vilitumwa kijijini mara moja baada ya kupokea taarifa za vurugu, wakipiga risasi hewani ili kutawanya umati. Uchunguzi wa pamoja umeanzishwa na IDF, Shirika la Usalama la Israeli, Shin Bet na polisi wa Israeli.
Marekani imelaani mashambulio na kusisitiza kuwa mamlaka za Israeli lazima zichukue hatua kulinda jamii zote na kuwawajibisha wahusika.
Wapalestina mara kwa mara wanalaumu majeshi ya usalama ya Israeli kwa kuruhusu makundi ya walowezi wenye vurugu kushambulia vijiji vyao.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (Ocha) imeripoti kuwa zaidi ya mashambulio 1,000 dhidi ya walowezi wa Kipalestina yamefanyika tangu Oktoba mwaka jana, yakiwemo 107 yaliyosababisha vifo na majeruhi kwa Wapalestina, na 859 yaliyosababisha uharibifu wa mali zao.
Marekani, Umoja wa Ulaya (EU), na Uingereza wameweka vikwazo dhidi ya baadhi ya viongozi wa walowezi na vituo vya walowezi kutokana na kiwango cha vurugu kilichoongezeka.
Imeandikwa kwa msaada wa mtandao.