Kisaka  ala shavu  Alliance | Mwanaspoti

BAADA ya kumaliza kozi ya Leseni ya Diploma A ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Kocha Ally Kisaka amelamba shavu kwa kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja na Alliance FC ya jijini hapa inayoshiriki First League.

Mzanzibari huyo aliyewahi kuzinoa Geita Gold, Pamba na Stand United aliisaidia Alliance FC kubaki kwenye ligi hiyo msimu uliopita baada ya kushinda mechi ya mtoano na kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu uliopita, lakini uongozi umembakisha.

Mwenyekiti wa Alliance, Stephano Nyaititi ameliambia Mwanaspoti kuwa wameridhishwa na kazi aliyoifanya kocha huyo kwa muda mfupi na kuwanusuru wasishuke daraja, ambapo msaidizi wake atatangazwa hivi karibuni.

“Maboresho ya benchi la ufundi timu ya wanaume yamefanyika. Sasa kazi tuliyonayo ni kuhakikisha tunampa ushirikiano ili afanye vizuri,” alisema Nyaititi.

Kuhusu usajili wa timu hiyo, Nyaitati alisema kwa sasa wamefikia asilimia 95 na wanapambana kuhakikisha timu inaanza kambi mapema kwani wana lengo la kuipandisha Championship.

Related Posts