RAIS SAMIA AWAKONGA MOYO SINGIDA MASHARIKI

  MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametembelea na kugua ujenzi wa miradi ya maji katika Kijiji Cha Mang’onyi ,mradi wa maji wa Kijiji cha Sakaa na Ujenzi wa Tanki la Maji katika Kijiji Cha Minyinga ambayo kukamilika kwake kutaondoa adha ya wananchi kutembea umbali mrefu kusaka maji. Akiwa katika Kijiji Cha Mang’onyi ambapo mradi…

Read More

Mafunzo ya usalama Osha ni zaidi ya darasa

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Saa nne za mafunzo ya usalama kazini kwa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (Jowuta) zilionekana hazitoshi kutokana na wengi kuwa na shauku ya kutaka kujifunza zaidi. Wako waliosikika wakisema ‘kumbe tunajimaliza wenyewe’, ‘nitanunua kiti changu niende nacho ofisini’, ‘nitaanza kubeba kipande cha mkaa kwenye mkoba wangu’ na…

Read More

Athari za watoto kwenda shule wakiwa na njaa

Dar es Salaam. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), limesema watoto wengi nchini Tanzania wanakwenda shuleni wakiwa na njaa. Mbali na hilo, Daktari wa binadamu, Edger Rutaigwa amesema lishe bora ni sehemu ya kinga ya magonjwa mbalimbali ya binadamu, akisisitiza lishe mbaya ndio chanzo cha maradhi mengi. Wamesema hayo leo…

Read More

Hospitali Amana yadhamiria kuokoa maisha ya watoto njiti

Na Nora Damian, Mtanzania Digital Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana imeanza kampeni ya kutafuta Sh bilioni 3 kwa lengo la kuboresha miundombinu na kununua vifaa tiba kuwaokoa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti). Hospitali hiyo inahudumia watoto wengi wanaozaliwa kabla ya wakati ambapo ina vitanda vidogo 80 na vitano tu vinavyomuwezesha mama kulala…

Read More

Faida za kupata kifungua kinywa kila siku asubuhi zatajwa

Dar es Salaam. Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) imeshauri umuhimu wa Watanzania kujijengea utaratibu wa kila asubuhi kuanza na kifungua kinywa kabla ya kuwahi kwenye majukumu yao, ili kupata nguvu ya kukabiliana na kazi zilizo mbele yao. Imesema bila kufanya hivyo hakuna mtu anayeweza kufanya kazi yeyote kwa ufanisi na kupata tija inayotakiwa…

Read More

Wanachama wa Chadema watahadharishwa ‘uchawa’

Dar es Salaam. Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema hali ya umaskini uliokithiri nchini kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, ni sababu ya kujikuta wakigeuka kuwa ‘chawa.’ Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 19, 2024 kwenye kongamano la Baraza la Wanawake (Bawacha) lililofanyikia Moshi, mkoani Kilimanjaro na Mwenyekiti…

Read More