Chemundugwao: Nipo tayari kujiunga Dar City

WAKATI timu ya Dar City ikiongoza Ligi ya Kikapu  Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), mchezaji nyota  wa zamani wa timu ya Dar City Trofimo Chemundugwao   anasema kuwa anategemea kujiunga timu yake hivi karibu

Chemundugwao ambaye yuko Mtwara kikazi, alisema atajiunga kikosini baada ya kumaliza kazi zilizompeleka Mtwara.

“Kazi karibu tunamaliza, nikitoka huku nitakwenda  moja kwa moja kujiunga na timu yangu ya Dar City,” alisema Chemundugwao .

Anasema akiwa mkoani Mtwara amekuwa akitumia muda mwingi kufanya mazoezi nyakati za jioni na wachezaji wa mkoani  huo.

“Kwa kweli kwa sasa najiona niko fiti,  kucheza mashindano yeyote,” alisema Chemundugwao.

Akizungumzia kuhusiana na ligi ya BDL, alisema amekuwa akiifuatilia na ameona kuna ushindani mkubwa.

Aidha, hakusita kupongeza timu zote kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya juu.

Ligi ya kikapu ya mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka mingi imekuwa ndio ligi yenye ushindani mkubwa zaidi nchini ukilinganisha na ligi za mikoa mingine.

Related Posts