Simba Queens yaambulia sare, kuikabili Kenya Police Bullets

Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya timu za soka za wanawakw ukanda wa Cecafa, Simba Queens wamemaliza kibabe mechi za makundi kwa kulazaimishwa sare ya 2-2 dhidi ya PVP Buyenzi ya Burundi.

Licha ya matokeo hayo tayari, Simba ilishafuzu nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ethiopia, baada ya kushinda michezo miwili ya awali ya Kundi B.

Simba imemaliza ikiwa pointi saba sawa na Kawempe Muslim Ladies ya Uganda inayoshika nafasi ya pili.

Katika nusu fainali Simba itacheza na Kenya Police Bullets, huku Kawempe Muslim Ladies ikikutana na wenyeji CBE ya Ethiopia. Bingwa wa michuano hiyo atafuzu Klabu Bingwa Afrika.