Wananchi wengi wa Gaza wanaishi katika makazi ya muda kutokana na mzozo huo.
Habari za Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeanza kukutana katika kikao cha dharura mjini New York kuhusu kuendelea mgogoro wa Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Hapo awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza makubaliano yamefikiwa na Israel kuruhusu kampeni kubwa ya chanjo ya polio kuendelea kupitia mfululizo wa mapumziko ya kibinadamu kuanzia Jumapili. Kwa watumiaji wa programu ya UN News, fuata moja kwa moja hapa.