MATI SUPER BRANDS LTD YAPEWA TUZO MAALUMU NA CHUO CHA UKAMANDA NA UNADHIMU (CSC) CHA JWTZ

Na Cathbert Kajuna – Kajunason/MMG. Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi yenye makao yake Makuu Mjini Babati Mkoani Manyara imepewa tuzo ya maalumu kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kushirikiana na taasisi mbali…

Read More

Maagizo ya Mkuu wa Wilaya Serengeti yatekelezwa

Na Malima Lubasha, Serengeti MAAGIZO aliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Kemirembe Lwota kwa uongozi wa Kijiji cha Nyami huru kilicho Kata ya Busawe ya kukutana na wananchi waliovamia eneo la kijiji la kujenga shule ya Sekondari na kuona jinsi ya kumaliza changamoto hiyo yametekelezwa kupitia vikao vya Kata,Tarafa na Kijiji. Utekelezaji wa maagizo hayo…

Read More

Mh.Sillo awajulia hali majeruhi wa ajali mkoani Manyara

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Daniel Sillo amesema Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za Kisheria madereva wote wasiotii na wanaokiuka sheria za usalama barabarani.   Mhe Sillo amezungumza hayo leo Agosti 31,2024 alipofika kuwajulia hali wanafunzi 30 wa shule ya sekondari Endasaki waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara baada…

Read More

NAIBU WAZIRI KAPINGA AMPONGEZA SPIKA WA BUNGE KUANDAA MASHINDANO YA KUPIKA KWA GESI YA ORYX MBEYA – MWANAHARAKATI MZALENDO

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amempongeza Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson kwa kuandaa mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kwa kushirikisha Mama na Baba Lishe 1000 kwani yamekuwa ya mfano na yametumika kutoa elimu ya nishati na utunzaji mazingira.   Ametoa pongezi hizo leo Agosti 31,2024 wakati akihitimisha mashindano hayo mkoani Mbeya ambapo…

Read More

Waliositisha masomo kwa ujauzito wasimulia machungu

Mwanza. Wasichana waliositisha elimu katika ngazi mbalimbali mkoani hapa, wameelezea changamoto wanazopitia ikiwemo unyanyapaa, kufukuzwa na kutolewa lugha chafu na ndugu zao. Hata hivyo, wanafunzi hao sasa wamepata matumaini baada ya kurejea katika mfumo wa elimu baada ya kupata mafunzo ya ufundi stadi. Wamesimulia machungu hayo leo Agosti 31, 2024 katika mahafali ya nane ya Chuo…

Read More

Mambo matatu kutawala kikao cha Kamati Kuu CCM kesho

Dar es Salaam. Hali ya kisiasa nchini na uteuzi wa mgombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki na maandalizi wa mkutano mkuu maalumu, ni miongoni mwa ajenda zinazotajwa kuchukua nafasi kwenye kikao cha Kamati Kuu Maalumu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kinachotarajiwa kufanyika kesho Septemba Mosi, 2024. Pia, ajenda nyingine inatajwa kuwa ni maandalizi ya…

Read More

PIGA MSHINDO LEO KWA KUBASHIRI NA MERIDIANBET

HUTAKIWI kupata mawazo unapata wapi pesa wikiendi hii kwakua mabingwa wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet wako kuhakikisha wikiendi yako inakua ya kibabe, Kwani kupitia michezo ambayo inakwenda kupigwa imepewa Odds za kutosha. Hakuna maelekezo mengine zaidi ya kufanya machaguzi yako kwa timu unazoamini zitakupatia kitita leo, Kwani ligi zote kubwa ulaya zimerejea leo…

Read More

TMDA yanasa vifaatiba, dawa bandia

Tabora. Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba nchini (TMDA) Kanda ya Magharibi,  imefanikiwa kukamata dawa na vifaa tiba ambavyo havijasajiliwa vyenye thamani zaidi ya Sh150  katika kipindi cha kuanzia Januari 2023 hadi Agosti 2024. Akizungumza na Mwananchi Agosti 30, Meneja wa kanda hiyo, Christopher Migoha amesema oparesheni zimekuwa zikifanyika kwa kushtukiza, jambo lililowafanya wanase dawa na…

Read More