
Mikoa mguu sawa, Riadha Taifa ikifunguliwa kesho
Mikoa imetambiana kutwaa ubingwa wa riadha kwenye mashindano ya Taifa yanayofunguliwa kesho Ijumaa jijini hapa. Tayari mikoa karibu yote imewasili jijini Mwanza tayari kwa mashindano hayo ya siku mbili yatakayofikia tamati keshokutwa Jumamosi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa baadhi ya mikoa wameeleza walivyojipanga kutwaa ubingwa wa msimu huu. Kocha wa mkoa Pwani, Elias Hotay…