
Watoto kupotea kwailipua Simiyu kwa maandamano, mmoja adaiwa kuuawa
Bariadi. Matukio ya watoto kudaiwa kutekwa na watu wasiojulikana katika Mji wa Lamadi, Wilaya ya Busega, Mkoa wa Simiyu yameibua vurugu baina ya wananchi na polisi, ambao walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza hali hiyo. Mvutano huo ulidumu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni ya leo Jumatano, Agosti 21, 2024. Katikati ya muda…