
Wanawake waongoza mashauri ya ndoa, familia
Dar es Salaam. Wanawake wametajwa kuwa mstari wa mbele kuripoti mashauri ya ndoa na kifamilia kuliko wanaume, sababu zikiwa ni ongezeko la talaka, kutafuta mirathi na matunzo ya watoto. Hayo yamo kwenye ripoti ya msaada wa kisheria ya mwaka 2023 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) leo Jumanne Agosti 20, 2024…