
RC Mtaka: Utakuwa uchaguzi huru na haki
Dar es Salaam. Misingi ya demokrasia na uwajibikaji inajengwa na uchaguzi huru na haki unaotarajiwa kushuhudiwa Novemba mwaka huu, ukihusisha kuchagua viongozi wa ngazi ya mtaa, vijiji na vitongoji. Uchaguzi huo unatoa fursa kwa wananchi kushiriki moja kwa moja katika kuchagua viongozi wanaowaongoza katika ngazi ya chini ya utawala, jambo linalochangia katika ujenzi wa Taifa…