Mwenza wako unamuomba ruhusa au unampa taarifa?
Dar es Salaam. βNiliwahi kufungiwa nje na mume wangu, akitaka nirudi nilikotoka, ilikuwa ngumu kumshawishi, nilikuwa kwenye msiba tena wa ndugu yake, yaani shemeji yangu, kisa tu niliondoka nyumbani bila kumuaga,” anaanza kusimulia Penina John. Mama huyo wa mtoto mmoja wa miaka 12 na mumewe, Nelson Jumanne anasema siku hiyo alimpigia simu mumewe hakupokea, akalazimika…