Wanamtandao Tanzania waibua mapya rushwa ya ngono

Dar es Salaam. Wanamtandao wa Kupinga na Kupambana na Rushwa ya Ngono nchini Tanzania wametaka kuondolewa kwa kifungu cha 10(b) kwenye mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya rushwa, ambacho kinahukumu mtu aliyetendewa udhalilishaji huo kwa kigezo cha kushawishi. Tamko la wanamtandao hao limetolewa leo Jumatano, Agosti 14, 2024, jijini Dar es Salaam na Mary Ndano,…

Read More

Sudan Kusini wajadili uwezekano wa kufanya uchaguzi Desemba – DW – 14.08.2024

Nchi hiyo changa zaidi duniani bado haijashiriki mchakato wa uchaguzi wa kidemokrasia ikiwa ni takribani miaka 13 tangu kile kinachoitwa uhuru wake uliopiganiwa kwa bidii kutoka kwa Sudan, hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa watu wake na jumuiya ya kimataifa. Katika taarifa ambayo imechapishwakatika ukurasa wa Facebook wa ofisi hiyo ya rais inaeleza, “Rais, pamoja na…

Read More

Angalizo latolewa kabla ya kufungwa Ziwa Victoria

Mwanza. Siku moja baada Serikali kuitaka Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) kuandaa mkakati wa kulifunga ziwa hilo, wadau wameshauri mambo ya kufanya kabla ya kulifunga. Ushauri huo umetokana na kauli ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexender Mnyeti aliyoitoa kwenye kongamano la Ukuzaji viumbe Maji jijini Mwanza, akiiagiza Taasisi ya Uvuvi ya…

Read More

Anayedaiwa jambazi auawa kwa risasi, sita wakimbia

Karagwe. Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa jambazi ameuawa na polisi wa doria akidaiwa kuvamia maduka mawili katika mji mdogo wa Omurushaka, Karagwe, mkoani Kagera. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Agosti 9, 2024, saa saba usiku. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, amethibitisha tukio hilo leo Jumatano, Agosti 14, 2024. Amesema watu hao wanaodaiwa kuwa…

Read More

Tamisemi kutangaza ratiba ya  uchaguzi Serikali za mitaa 

Dodoma. Kipenga cha uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2024, kitapulizwa kesho Alhamisi, Agosti 15, 2024 wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohammed Mchengerwa atapotoa tangazo la uchaguzi huo. Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tamisemi, Nteghenjwa Hosseah, tangazo hilo litatolewa…

Read More

Utekaji wa bodaboda, ukatili vyaibuka ziara ya Dk Nchimbi Geita

Geita. Malalamiko ya madereva wa bodaboda kutekwa na kuporwa pikipiki zao, mauaji ya watoto wakiwamo walemavu ndiyo vilivyotawala kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi mkoani Geita. Kiongozi huyo wa chama akiwa anahitimisha ziara yake mkoani Geita alikutana na  kero mbalimbali zikiwamo za  mauaji ya watoto wakiwamo wenye ulemavu…

Read More

Mwanamke auawa Tabora, afichwa uvunguni

Tabora. Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamume kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga mkazi wa Mtaa wa Maselele, Kata ya Cheyo B  Manispaa ya Tabora, Juliana Mbogo (40) kisha mwili wake kuuficha uvunguni mwa kitanda, chanzo kikidaiwa ni wivu wa mapenzi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema hayo leo Jumatato, Agosti 14, 2024…

Read More