
Mawaziri 70 kujadili uvuvi, uchumi wa buluu Dar
Dar es Salaam. Mawaziri 70 kutoka mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) wanatarajia kukutana kwa siku tano nchini kujadili uchumi wa buluu na kuweka mkakati wa pamoja kuimarisha sekta ya uvuvi. Mkutano huo utakwenda sanjari na kongamano la kimataifa kuhusu mikakati ya Uboreshaji wa Mnyororo wa Uzalishaji wa Vyakula vya Majini…