Pamba Jiji ilivyojipanga kurejesha hadhi yake
PAMBA Jiji maarufu kama TP Lindanda ‘Wana Kawekamo’ wanarudi Ligi Kuu baada ya miaka 23 tangu waliposhuka daraja mwaka 2000, na Ijumaa itacheza mchezo wake wa kwanza wa michuano hiyo itakapofungua pazia la Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Pamba ni miongoni mwa timu zenye umaarufu na historia…