Kamanda wa zamani wa LRA atiwa hatiani kwa uhalifu Uganda – DW – 14.08.2024
Uamuzi uliosubiriwa kwa muda mrefu katikakesi ya Thomas Kwoyelo ulitolewa Jumanne na jopo la Mahakama Kuu lililoketi Gulu, mji wa kaskazini ambapo LRA ilikuwa inaendesha uasi wake. Ilikuwa ni kesi ya kwanza ya ukatili kuhukumiwa chini ya kitengo maalum cha Mahakama Kuu ambacho kinaangazia uhalifu wa kimataifa. Kwoyelo alikabiliwa na mashtaka yakiwemo mauaji, wizi, utumwa,…