Wataalamu 250 wa afya ulimwenguni kukutana Tanzania

Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la Kisayansi la Kimataifa la Matumizi ya Mawimbi Sauti katika Tiba (ISMRM) pamoja na Tiba ya Mishipa ya Fahamu (Neuroradiology) litakalofanyika Septemba 19 hadi 20, 2024 jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limeratibiwa nchini na Chama cha Madaktari Bingwa wa Rediolojia Tanzania (Taraso); Chama cha Wataalamu…

Read More

Serikali mbioni kufunga Ziwa Victoria

Mwanza. Ikiwa imebaki siku moja Ziwa Tanganyika lifunguliwe Agosti 15, 2024, Serikali imewataka wasimamizi wa Ziwa Victoria kuandaa mkakati wa kulifunga. Ziwa Tanganyika lilifungwa Mei 15, 2024, ili kutoa nafasi kwa ziwa hilo kupumzika na mazao ya uvuvi kuzaliana na kuongezeka ziwani. Akizungumza leo Jumanne Agosti 13, 2024, kwenye ufunguzi wa kongamano la Ukuzaji viumbe…

Read More

Kilio wizi mita za maji Manispaa ya Iringa

Iringa. Wakazi wa Manispaa ya Iringa wamelalamikia ongezeko la wizi wa mita za maji unaoendelea katika manispaa hiyo, hali inayosababisha hasara kubwa kwa kulazimika kununua mita nyingine kila wakati. Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Agosti 13, 2024, wananchi hao wamesema wizi huo umekuwa ukitokea katika mitaa ya Mawelewele, Kihesa, Mkwawa, Gangilonga na maeneo mengine,…

Read More

Viongozi wa dini walaani mauaji ya mtoto Amedeus

Rombo. Wakati mwili wa mtoto Amedeus Laurent(7), ukizikwa leo Agosti 13, 2024  nyumbani kwao Kijiji cha Mahango, Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, viongozi wa dini na wadau wa haki za binadamu wamelaani mauaji ya watoto yanayoendelea nchini. Hata hivyo, wanafunzi wa shule alikokuwa akisoma mwanafunzi huyo, wamekuja na  mabango kwenye maziko ya mwenzao yakiwa yameandikwa…

Read More

Kesi ya mtoto wa Askofu Sepeku kuunguruma Sept 19

Dar es Salaam. Kesi ya Bernardo Sepeku ambaye ni mtoto wa marehemu John Sepeku aliyekuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa Kanisa Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea kutokana na jaji anayesikiliza shauri hilo kuwa na majukumu mengine ya kikazi. Bernado alifungua kesi ya madai Mahakama Kuu, Divisheni ya Ardhi, akipinga kunyang’anywa zawadi…

Read More

Uchakataji usiofaa unavyoharibu soko la dagaa Mwanza

Mwanza. Baadhi ya wajasiriamali jijini Mwanza wamelalamikia uchakataji holela wa dagaa, wakisema unaharibu soko la kitoweo hicho. Wamesema uchakataji unaofanywa na baadhi yao, hauzingatii ubora, badala yake umejikita kwenye tamaa ya fedha, jambo linalopunguza imani ya wateja. Wajasiriamali hao wamesema hayo jana Jumatatu Agosti 12, 2024 wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo (MSMEs)…

Read More

Takukuru yawatolea macho wanasiasa | Mwananchi

Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kilimanjaro, imewaonya wanasiasa mkoani humo walioanza kujipitisha mitaani na kutoa pombe, vyakula na zawadi ndogondogo ili kuwashawishi wananchi kuwachagua wakati wa uchaguzi. Imewataka wanasiasa hao kuacha mara moja vitendo hivyo, kwa kuwa ni sehemu ya rushwa na vinachangia kupatikana kwa viongozi wasio sahihi. Rai…

Read More