Wahitimu mafunzo ya amali watakiwa kuanzisha vikundi wakopeshwe
Unguja. Wakati Serikali ikiendelea kuongeza vyuo vya mafunzo ya amali, wahitimu wametakiwa kuunda vikundi ili wapatiwe mikopo isiyo na riba kujiendeleza kiuchumi. Hayo yameelezwa leo Agosti 12, 2024 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Muhamed Mussa katika mahafali ya 11 ya Chuo Cha Mafunzo ya Amali (VTA) Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja….