
Manaibu gavana Kenya walalamikia kutokuwa na kazi – DW – 29.08.2024
Manaibu Gavana hao wakiongozwa na Naibu Gavana wa Laikipia Reuben Kamuri wanasema magavana wengi wanawakabidhi wasaidizi wao wakuu majukumu yao na kuwaacha wao bila kazi. Manaibu wa magavana hao wamefika mbele ya kamati ya bunge la Seneti inayosimamia masuala ya ugatuzi ambapo wamewasilisha ombi la kutaka kubadilishwa kwa sheria ya usimamizi wa serikali za kaunti…