Wahamiaji haramu wadakwa dereva atelekeza gari, atokomea

Arusha. Wakati wimbi la wahamiaji haramu likiendelea kutikisa nchini, wahamiaji saba raia wa Ethiopia na Somalia walioingia nchini kwa njia za panya, wamekamatwa wakiwa wamejificha kwenye shamba la mahindi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Agosti 12, 2024 na Jeshi la Uhamiaji mkoani Arusha kupitia kwa Ofisa Uhamiaji, Fakih Nyakunda amesema waliwakamata wahamiaji hao…

Read More

MARIOO ASHINDA KESI YA MADAI ALIYOTAKIWA KULIPA MILIONI 500 – MWANAHARAKATI MZALENDO

  Mahakama Kuu Arusha imeitulipia mbali Kesi iliyokuwa inamkabili msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Omary Ally Mwanga alimaarufu kama Marioo.     Katika kesi hiyo Marioo alishtakiwa yeye pamoja na meneja wake Sweetbert Charles Mwinula na Kampuni ya Kismaty Advert Media Co. Ltd, Kampuni inayojihusisha na uandaaji wa matamasha na shughuli zinazohusiana na burudani…

Read More

Upelelezi kesi ya aliyejitambulisha Profesa Kamugisha wa Muhimbili bado

Dar es Salaam. Uchunguzi bado unaendelea katika kesi ya kutakatisha fedha na kujipatia Sh7.3 milioni kwa udanganyifu inayomkabili mfanyabiashara Ibrahim Bigirwa (33) na wenzake wawili. Bigirwa na wenzake, wanakabiliwa na mashtaka 50, yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, kujipatia fedha kwa udanganyifu kutoka kwa watu mbalimbali. Bigirwa  pekee, anakabiliwa na mashtaka ya kujitambulisha kwa watu…

Read More

Mzize: Chama ana jicho la pasi

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize amesema ubora wa pasi ya mwisho ya Clatous Chama ulimpa urahisi wa kukwamisha mpira nyavuni. Mzize alifunga bao la nne na la mwisho kwenye ushindi wa mabao 4-1 ilioupata Yanga dhidi ya Azam katika fainali ya Ngao ya Jamii iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Mabao…

Read More

AMREF TANZANIA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI – DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunga maadhimisho ya siku ya vijana kitaifa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma. Mbali na mambo mengine, Waziri Ridhiwani Kikwete ametembelea banda la Amref Tanzania na kuelezwa namna AmrefTanzania inavyounga mkono juhudi za serikali katika…

Read More

Ombi la Wahifadhi wa Ndovu kwa Marais Ruto na Suluhu Kuhusu Ushirikiano wa Mipakani Kuhusu Ulinzi wa Tembo – MWANAHARAKATI MZALENDO

Wanasayansi na wahifadhi wa mazingira, leo, siku ya Ulinzi wa Tembo/Ndovu Ulimwenguni, wameikabidhi serikali ya Tanzania arafa la ombi la kimataifa la sahihi zaidi ya 500,000 inayonuiwa kuwarai kutamatisha uwindaji wa ndovu katika maeneo yake yanayopakana na Kenya. Hii ni kutokana na hatua ya utawala wa Tanzania kutoa vibali vya uwindaji wa ndovu wenye pembe…

Read More