MTU WA MPIRA: Simba Imesajili vizuri, Yanga bado ni bora
TUMESHUHUDIA Dabi ya Kariakoo bora kabisa Alhamisi iliyopita. Soka lilipigwa kweli kweli pale kwa Mkapa. Hakuna aliyetaka kupoteza hata sekunde. Licha ya ushindi wa Yanga, mpira ulikuwa mzuri sana. Ulikuwa wa ushindani na ufundi mkubwa. Uliakisi ukubwa wa soka la Tanzania kwa sasa. Kabla ya mchezo Yanga alipewa nafasi kubwa ya kushinda. Wapo walioamini angeshinda…