Wakazi Ngara walia upatikanaji wa vitambulisho vya Nida, maji
Ngara. Wakazi wa Kijiji cha Kumunazi kilichopo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, wameeleza kero ya kutopatiwa vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), jambo linalowakwamisha kupata baadhi ya huduma muhimu. Wakazi hao wameeleza hayo leo Jumatano Agosti 7, 2024 mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi…