Kamanda Muliro: Tupo hatua za mwisho za uchunguzi ‘waliotumwa na afande’
Dar es Salaam. Jeshi Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema upelelezi wa tukio la binti anayedaiwa kubakwa na kulawitiwa kisha video yake ikasambazwa katika mitandao ya kijamii upo hatua za mwisho. Sambamba na hilo, jeshi hilo limekanusha taarifa ilizodai za uzushi kuhusu kifo cha binti aliyefanyiwa ukatili huo, likidai yupo hai. Video za…