Baba mzazi wa aliyechoma picha ya Rais amtaka mwanawe akiwa hai au mfu
Mbeya. Mkazi wa Kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Yusuph Chaula (56) amemwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la mwanawe Shadrack Chaula kutekwa na watu wasiojulikana. Shadrack anadaiwa kutekwa na watu hao Agosti 2, 2024 ikiwa ni takribani siku 20 kupita tangu alipotoka Gereza la Ruanda Mkoa lililoko mkoani Mbeya, alipokuwa…