
Jamhuri yafurika wananchi, askari wafunga milango, Rais Samia apiga ‘selfie’
Morogoro. Umati mkubwa wa wananchi umejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kuhudhuria mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu Hassan. Mkutano huo umefanyika leo Jumanne, Agosti 6, 2024 ukihitimisha ziara ya Rais Samia mkoani humo aliyoianza Agosti 2, 2024. Katika siku hizo amezindua, kuweka mawe ya msingi ya miradi mbalimbali ya maendeleo….