TTCL YATINGA NANENANE 2024 .

  Shirika la Mawasiliano Tanzania -TTCL ni miongoni wa Wadau wanaoshiriki katika maonesho ya 31 ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nanenane Nzuguni, jijini Dodoma kuanzia tarehe Agosti 1 hadi Agosti 8,2024. Shirika hilo linashiriki kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanaotembelea maonesho ya Nanenane wanapata elimu kuhusu huduma na bidhaa zinazotolewa na…

Read More

Mageti yaongezwa Kwa MKapa kupunguza msongamano

MENEJIMENTI  ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, umejiongeza ili kuwarahisisha kazi mashabiki wa Simba waliojitokeza kushangweka na Tamasha la Simba Day, baada ya kuongeza mageti zaidi ya kuingilia uwanjani baada ya kuibuka malalamiko ya mashabiki walioidai wamekaa muda mrefu katika foleni ya kuingia ndani. Awali mashabiki waliokata tiketi kwa ajili ya kuingia uwanjani kushuhudia Tamasha la…

Read More

Rais Samia ataja kitakachowaingiza Gen Z barabarani

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesema kutokuwepo kwa chakula ndiko kutawafanya vijana wa kizazi cha Z maarufu Gen Z, waingie barabarani. Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo wakati akielezea umuhimu wa Serikali kusimamia masilahi ya makundi yote katika jamii. Ameyasema hayo leo Jumamosi, Agosti 3, 2024 alipozindua bwawa la umwagiliaji la Kiwanda…

Read More

Mastaa NBA walivyoibeba Olimpiki 2024

VITA ya mashindano ya Olimpiki kusaka medali ya dhahabu ya mchezo wa kikapu jijini Paris, Ufaransa inaendelea kuwa moto upande wa makundi, ambapo wababe wawili walioupiga mwingi ni kutoka ukanda unaochezwa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ikiwa ni pamoja na Canada. Canada ilifanikiwa kushinda mechi zote tatu juzi Ijumaa ilipoifunga Hispania 88-85 ikisonga hatua ya…

Read More

Hivi ndivyo TLS ya Mwabukusi itakavyokuwa

Dar es Salaam. Kufuata ushindi alioupata, Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amesema atakirudisha chama hicho kwenye misingi yake. Katika uchaguzi huo uliofanyika jijini Dodoma Agosti 2, 2024 Mwabukusi aliibuka mshindi kwa kupata kura 1,274 kati ya 2,218 zilizopigwa akifuatiwa na Sweetbert Nkuba aliyepata kura 807. Wagombea wengine katika uchaguzi huo…

Read More

Ukilipa zaidi ya hapo kupata saini zao, umepigwa

LONDON, ENGLAND: DIRISHA la usajili wa mastaa huko Ulaya bado halijafungwa na klabu mbalimbali bado zipo bize kwenye kuhakikisha zinanasa saini za wachezaji wapya ili kwenda kuboresha vikosi vyao. Tayari kuna timu zimepata wachezaji zilizokuwa zikiwahitaji ili kwenda kufanya vikosi vyao kuwa imara zaidi, huku timu nyingine zikiwa bado sokoni kusaka mastaa ambao zinaamini zikiwapata…

Read More

Foleni Simba Day balaa! | Mwanaspoti

‘UBAYA UBWELA’ hadi kieleweke zimesikika sauti za mashabiki wa Simba ambao wamekaa katika nguzo za umeme wakisubiri foleni ya kuingia uwanjani. Nguzo hizo za chuma zimelazwa chini mita chache kutoka Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo kunafanyika shughuli ya kilele cha tamasha la Simba Day. Unaambiwa, kutokana na msururu wa mashabiki wengi waliopanga mstari kuingia ndani…

Read More

Simba Day, Kwa Mkapa yageuka gulio

SIMBA hawana jambo dogo, achana na nyomi la watu waliokuwa wanaingia uwanjani kushuhudia timu hiyo ikiadhimisha kilele cha siku ya Simba Day lakini uwanjani hapo ni kama pamegeuka gulio. Leo Simba inaadhimisha Tamasha la Simba Day ambayo imepewa jina la Ubaya Ubwela ikiambatana na burudani ya mechi ya kirafiki kati ya Simba na APR ya…

Read More

Kwa Mkapa ni nyekundu na nyeupe

ZIKIWA zimebaki saa nane kabla ya wana Simba kushuhudia kikosi kipya cha msimu wa 2024/25, hapa Benjamin Mkapa Ubaya Ubwela ni mwingi, hii ni baada ya jezi nyekundu na nyeupe kutapakaa karibu kila kona nje ya uwanja. Rangi hizo ndizo zinazotumiwa zaidi na Simba katika jezi za klabu hiyo, jambo linaloashiria mashabiki wa timu hiyo…

Read More