
Kiongozi wa Hamas kuzikwa Qatar – DW – 02.08.2024
Mwili wa Ismail Haniyeh uliwasili tangu jana Alhamisi katika mji mkuu wa Qatar, Doha tayari kwa mazishi na baadhi ya picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha mkewe Amal akiomboleza kwenye jeneza la mumewe kabla ya kuzikwa. “Wewe ni msaada wangu kwenye maisha ya sasa na ya baadae. Kipenzi changu. Wasalimie mashahidi wa Gaza, wasalimie…