
SIMULIZI YA HADITHI: Jana dume – 4
ILIPOISHIA… Nikahisi alikuwa mzungu mwenyeji kwani alikuwa akiifahamu vyema lugha ya Kiswahili. “Bila samahani, niombe tu.” Nikamjibu. “Lakini natanguliza samahani, sijui kama utaridhika.” Aliponiambia hivyo nilishituka kidogo. “Kwani unataka kuniomba nini?” SASA ENDELEA… “NAOMBA namba yako.” “Namba yangu ya….?” “Nilikuwa na maana namba yako ya simu.” “Kama ni hilo tu hakuna tatizo.” Nikamwambia. Nikampa namba…