Morocco: Stars ipo kamili gado

KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleimani ‘Morocco’ amesema, kikosi hicho kiko kamili kwa ajili ya michezo miwili ya kimataifa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), itakayofanyika mwakani. Stars iliyopo kundi ‘H’ la kutafuta nafasi ya kufuzu michuano hiyo, itashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini…

Read More

Rufaa yawanasua wawili waliohukumiwa kunyongwa

Arusha. Mahakama ya Rufani iliyoketi Mwanza, imewaachia huru Fikiri Kalamji na Samwel Kalamji, waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mama yao mzazi, Pili Ndulu ili warithi mali zilizoachwa na baba yao. Fikiri na Samwel walihukumiwa adhabu hiyo na Mahakama  Kuu Kanda ya Geita, Disemba 24, 2020, ambapo walidaiwa kumuua mama…

Read More

Wabunge wapewa tahadhari sheria ya rushwa ya ngono

Dar es Salaam. Wakati muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ukitarajiwa kuwasilishwa bungeni Septemba 2, 2024, mtandao wa kupinga rushwa ya ngono, umewataka wabunge kutoupitisha wakidai unalenga kuwanyamizisha waathirika na kuwapa nguvu wenye mamlaka wanaofanya vitendo hivyo. Kwa mujibu wa mtandao huo, kifungu cha 10(b) ambacho kimeongezwa kwenye mabadiliko ya…

Read More

CRDB Bank Foundation yazindua Kampeni ya Kuwaunganisha Wajasiriamali Wadogowadogo nchini na programu ya IMBEJU

   Dar es Salaam, 30 Agosti 2024 – Taasisi ya CRDB Bank Foundation imezindua rasmi kampeni maalum ya IMBEJU inayolenga kuwaunganisha vijana na wanawake wajasiriamali nchini na programu ya IMBEJU. Hafla hiyo ya uzinduzi ilifanyika katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na washirika wa programu hiyo. Akizungumza Mkurugenzi…

Read More

4R za Samia zitakavyochochea uchaguzi huru na haki

Dar es Salaam. Tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, ameonyesha dhamira ya kuimarisha demokrasia na utawala bora nchini kupitia falsafa ya 4R. Falsafa hiyo inahusisha mageuzi ya kiutawala na kisiasa ili kuhakikisha Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya haki, uwazi na uwajibikaji. Kwa muktadha wa uchaguzi wa serikali za mitaa, 4R za Rais Samia zina…

Read More

Afungwa maisha jela kwa kumlawiti mtoto wa miaka miwili

Mbulu. Mkazi wa kijiji cha Moringe, mkoani Manyara, Carol Christopher (18) amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama ya Wilaya ya Mbulu kwa kumlawiti mtoto wa miaka miwili na miezi nane. Hata hivyo, Carol hakuwepo mahakamani wakati wa hukumu hiyo iliyotolewa Agosti 30 na kusababisha mama yake ambaye ni mdhamini wake kuhukumiwa miezi sita gerezani….

Read More

Mwenyekiti wa mtaa apiga magoti kuwaomba msamaha wananchi

Mwanza. Katika hali isiyo ya kawaida, mwenyekiti wa Mtaa wa California uliopo katika kata ya Nyegezi jijini Mwanza, Fadhili Nassoro amewapigia magoti wakazi wa mtaa huo, akiwaomba msamaha kwa makosa aliyowafanyia kwa kujua ama kutojua wakati wa uongozi wake. Nassoro amechukua hatua hiyo Agosti 30, 2024 ikiwa imesalia miezi mitatu ya kukabidhi muhuri wa ofisi…

Read More