
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 27,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 27,2024 About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 27,2024 About the author
Geita. Hukumu ya kesi ya mauaji ya Milembe Suleman iliyotarajiwa kutolewa leo, Agosti 26, 2024, imeahirishwa na sasa itasomwa kesho, Agosti 27, 2024, saa tatu asubuhi. Sababu zilizotajwa za kuahirishwa kwa hukumu hiyo ni urefu wa kesi, wingi wa mashahidi, pamoja na mchakato wa utafutaji wa haki kwa pande zote mbili. Jaji mfawidhi wa Mahakama…
Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametaja sababu tatu za kuanzisha Kampeni ya ‘Dawasa mtaa kwa mtaa, njoo tukuhudumie’ ikiwemo kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuondoa lawama na manung’uniko na kuwapatia huduma ya maji safi na salama. Kampeni hiyo itakayosambaa nchi nzima inalenga kuwa karibu na wananchi, ili wawe huru kutoa maoni yao…
Dar es Salaam. Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa elimu ya fedha na umuhimu wa kuweka akiba kwa wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Pugu, iliyopo Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam. Hatua hii inalenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa kifedha, kuwawezesha kujiwekea akiba, kubuni mawazo ya biashara na kufahamu jinsi…
Moshi. Dickson Sambo (37), anayeugua ugonjwa wa figo na anahitaji Sh50 milioni kwa ajili ya kupandikiza figo mpya, amefanikiwa kupata Sh9 milioni hadi sasa. Hata hivyo, bado anahitaji Sh41 milioni ili kufanikisha matibabu hayo. Sambo, mkazi wa Mbokomu Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, figo zake mbili zilifeli miaka minane iliyopita, baada ya kupatwa na shinikizo…
Dar es Salaam. Kutokana na ufinyu wa eneo katika Kituo cha Afya cha Tandale ambao unasababisha changamoto katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi, kituo hicho kiko mbioni kuongezwa ukubwa. Kwa sasa, kituo hicho kinakadiriwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya 1,000 kwa siku, sawa na watu 30,000 kwa mwezi, kama alivyoeleza Mganga Mfawidhi wa kituo…
Mufindi. Wakati mgomo wa wafanyabiashara katika soko kuu Mafinga mkoani Iringa ukiinga siku ya nne nne leo, wafanyabiashara wa matunda, nafaka pamoja na samaki wamelalamikia wakisema mgomo huo unawaathiri kibiashara. Mgomo huo umesababisha adha kwa wananchi na wafanyabiashara wasio na maduka, wakisema wanayategemea maduka hayo kupata bidhaa za kuuza. Mwenyekiti wa soko hilo, Philinus Mgaya…
Dar es Salaam. Benki ya CRDB kwa kushirikiana na kampuni ya malipo ya Visa International imetangaza kutoa nafuu ya nauli ya asilimia 22 kwa abiria wa Shirika la Ndege la Qatar watakaolipia tiketi zao kwa kutumia kadi za Tembocard Visa. Nafuu hiyo inajumuisha punguzo la asilimia 12 litakalotolewa na kampuni ya Visa International pamoja na…
Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kunduchi Mheshimiwa Michael Urio amefanya ziara ya kushtukiza kwenye mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Abbas Tarimba leo Agosti 26, 2024 sambamba na kutembelea Kituo cha afya cha Tandale kwa lengo la kusikiliza na kuzitatu changamoto zilizopo kwenye kituo hicho….
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Peter Msofe amedokeza kuanza kutumikia kwa mtalaa mmoja kwa wanafunzi wa masomo ya udaktari na uuguzi, lengo likiwa kupata wahitimu wenye sifa moja na washindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi. Pia kuanza kutumika kwa mtalaa huo kutawaongezea…