
DC ajitosa kumsaidia mwanafunzi aliyeacha shule alee wadogo zake
Njombe. Siku moja baada ya Mwananchi kuripoti taarifa kuhusu Sarah Chaula (17), mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Ilumaki, wilayani Makete Mkoa wa Njombe, aliyeacha masomo ili awalee wadogo zake wawili, Nuru Chaula (13) na Faraja Chaula (10), hatimaye Serikali ya Wilaya ya Makete imeingilia kati. Mtoto huyo mkazi wa Kijiji cha…