
Wanafunzi sita wadaiwa kufariki dunia kwa kunasa kwenye tope wakiogelea
Wanafunzi sita wa Shule ya Msingi Ochuna Wilaya ya Rorya mkoani Mara wamefariki dunia wakidaiwa kuzama na kunasa kwenye tope katika bwawa la skimu ya kilimo cha umwagiliaji lililopo kijijini hapo. Watoto hao wakiwemo watatu wa familia moja wote ni wakazi wa kijiji cha Ochuna. Tukio hilo limetokea jana Jumamosi Agosti 24, 2024 jioni baada…