
Hatari utamaduni wa ‘ndugu’ kujamiiana ukianza kuota mizizi
Kwa mzazi inaweza isikuingie akilini kwamba watoto wako unaoishi nao nyumba moja wanaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi, ila ukweli uko hivyo, yapo matukio mengi ya aina hiyo ambayo yanaendelea kushika kasi kwenye jamii. Hii inahusisha ndugu wa damu, ndugu wa familia au ukoo na hata baba na mtoto ambayo kwa tamaduni zetu wanaitwa maharimu….