
Mgomo wa wafanyabiashara Mafinga waingia siku ya pili
Mufindi. Mgomo wa wafanyabiashara katika Soko Kuu la Mafinga lililopo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wa kufunga maduka, umeingia siku ya pili leo Agosti 24, 2024 ukisababisha adha kwa wananchi kukosa huduma. Mwananchi limefika sokoni hapo na kushuhudia milango ya maduka hayo imefungwa huku baadhi ya wananchi waliofika kwa ajili ya kupata huduma wakiduwaa wasijue…