
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 2,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 2,2024 About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 2,2024 About the author
Dar es Salaam. Wakati maandalizi ya chaguzi zijazo yakiendelea nchini, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea, Damian Dallu ameonyesha hofu kwa yanayoendelea kama yatachagiza kupata viongozi bora. Kiongozi huyo wa kiroho amewataka Watanzania katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 kutafuta mtu atakayewasaidia na kutanguliza mbele utu…
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Longido (DC), Marco Ng’umbi baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja na miezi minane katika wilaya hiyo. Ingawa taarifa ya Ikulu iliyotolewa jioni ya leo Jumapili, Septemba mosi, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga, haikuweka wazi sababu…
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam. Kamati Kuu Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imewateua makada wake 10 kugombea ubunge wa Afrika Mashariki (EALA), kurithi nafasi iliyoachwa wazi na Dk Shongo Sedoyeka aliyefariki dunia Juni 13, 2024. Hata hivyo, uamuzi huo wa kamati kuu umewakata makada wengine 37 waliotia nia kuomba ridhaa ya chama hicho kuteuliwa kugombea ubunge…
Tabora. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amemtaka Waziri kivuli wa katiba na sheria wa chama cha ACT- Wazalendo, Maharagande Mbarala, kuthibitisha tuhuma alizotoa kuhusu mauaji ya watu wilayani Kaliua. Pia amemtaka kuthibitisha tuhuma za kuwapo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu katika vijiji 11 vyenye mgogoro wa ardhi unaofanywa na wenye mamlaka. Akizungumza…
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwezekano wa kutokea kwa upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa, kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Jumapili Septemba 1 hadi 3, 2024 katika baadhi ya mikoa nchini. Upepo huo unatarajiwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa kusini mwa Ziwa…
Watumishi wa Wakala wa Vipimo wakifanya mazoezi ya viungo kabla ya kushiriki katika michezo mbalimbali …… Ikiwa imebaki miezi miwili kuelekea mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi ( SHIMUTA) ambayo yamepangwa kufanyika katika Viwanja vya CCM Mkwakwani mkoani Tanga kuanzia tarehe 10 hadi 24 Novemba,2024, Wakala wa Vipimo (WMA)imefanya…
Babati. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amesema Serikali itagharamia matibabu kwa wanafunzi majeruhi wa ajali ya magari mawili yaligongana na kusababisha vifo vya watu wanne jana. Sendiga ameyasema hayo leo Jumapili Septemba Mosi, 2024 baada ya kuwatembelea majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa Hospitalini ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, mjini Babati. Ajali…
WAKATI benchi la ufundi Ken Gold likiahidi kusuka kikosi upya, uongozi wa timu hiyo nao umekoleza moto kwa mastaa ukiahidi dau nono kwa matokeo ya ushindi kuanzia mchezo ujao dhidi ya Fountain Gate. Ken Gold inayoshiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza haijaanza vyema msimu, baada ya kupoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Singida Black…