
Rais Abdelmadjid Tebboune ashinda muhula wa pili Algeria – DW – 09.09.2024
Katika matokeo ambayo yaliwashangaza waangalizi wachache kimataifa na hata ndani ya Algeria kwenyewe, tume huru ya uchaguzi nchini humo ilitangaza Jumapili kwamba Tebboune ameshinda asilimia 94 ya kura, akiwazidi wapinzani wake, mgombea wa chama cha Kiislamu, Abdelali Hassani Cherif, aliyepata asilimia 3 pekee na msoshalisti Youcef Aouchiche, ambaye aliambulia asilimia 2.1. Maafisa wa uchaguzi wameripoti kuwa…