Hali ilivyo Kituo cha Polisi Lulembela kilichovamiwa na wananchi

Picha za hali ya kituo cha Polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita baada ya jana Jumatano Septemba 11, 2024 kuvamiwa na wananchi huku wakifanya uharibifu wa baadhi ya mali ikiwamo gari.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime katika taarifa yake jana Jumatano kuhusu tukio hilo, alisema chanzo cha vurugu hizo ni baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa kwenye mnada wa Lulembelea kuwadhania ni wezi wa watoto kisha  kuwashambulia.

“Walipokuwa wanawashambulia alitokea ofisa mtendaji wa kata  akawabeba kwenye pikipiki na kuwapeleka katika Kituo cha Polisi Lulembela baada ya watu hao kwenye gari, akawapeleka kituoni, hata hivyo wananchi takribani 800 walifika kituoni na kuwataka polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue,” amedai Misime.

Amesema licha ya askari polisi kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa kujichukulia sheria mkononi, wananchi hao walikaidi na kuanza kukishambulia kituo cha polisi kwa mawe wakilazimisha kuwachukua watu hao wawili kwa nguvu ili wawaue.

Gari lililochomwa moto na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Lulembela  

Gari lililochomwa moto na wananchi nje ya Kituo cha Polisi Lulembela  

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa katika eneo Lulembela  

Baadhi ya maduka yakiwa yamefungwa katika eneo Lulembela