PLANET imeendeleza moto katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza kwa kuifunga timu ya Profile kwa pointi 49-45 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mirongo, jijini humo.
Katika mchezo huo, John Pastory aliongoza kwa kufunga pointi 26, aliongoza pia kwa kutoa asisti mara 7 na upande wa udakaji (rebounds) alidaka mara 7.
Katika mchezo mwingine uliochezwa uwanjani hapo, timu ya CUHAS iliifunga Oratori kwa pointi 58-46.
Isanchu Mrimba wa timu ya CUHAS alifunga pointi 10, aliongoza kwa kudaka mipira ya rebounds mara 14 na alizuia (blocks) mara moja.
Timu zinazoshiriki katika ligi hiyo ni Sengerema Hoopers, CUHAS, Oratori, Profile, Young Profile, Mwanza Eagles, Planet na CIC.