Rais wa Guinea Bissau atangaza kutogombea muhula wa pili – DW – 12.09.2024

Angela Mdungu

12 Septemba 2024

Rais wa Guinea Bissau Umaro Cissoko Embalo ametangaza hivi leo kuwa hatowania muhula wa pili katika uchaguzi wa Novemba. Embalo, mwenye umri wa miaka 51, alichaguliwa Januari 2020 akimrithi rais Jose Mario Vaz.

https://p.dw.com/p/4kYk8

Rais wa Guinea Bissau Umaro Cissoko Embalo
Rais wa Guinea Bissau Umaro Cissoko Embalo.Picha: Alexei Maishev/TASS/dpa/picture alliance

Alimshinda Domingos Simoes Pereira akiwa na asilimia 54 ya kura na alistahili muhula mwingine madarakani.

Tangazo lake la kushutukiza linaweza kusababisha ombwe la uongozi na kuzidisha machafuko ya kisiasa katika nchi hiyo iliyowahi kutikiswa na mapinduzi yenye wakaazi takriban milioni mbili. 

Soma pia:Rais wa Guinea-Bissau amfuta kazi mkuu wa majeshi kwa jaribio la mapinduzi

Embalo, aliingia madarakani wakati kukiwa na mgogoro wa kisiasa wa muda mrefu katika nchi ambayo mapinduzi na machafuko yamekuwa ni ya kawaida tangu ilipopata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974.