Wakati timu za kikapu za wanawake zikiendelea kuchuana vikali katika Ligi ya Likapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), imeonyesha wachezaji wanaotokea katika kituo cha Ukonga Academy ndiyo wanaotawala ligi hiyo.
Licha ya timu nyingine kuwakilishwa na wachezaji wenye viwango vya juu, imeonekana wengi wa wachezaji hao wanatokea katika kituo hicho.
Baadhi ya wachezaji waliotokea kituo hicho ni Noela Renatus, Hafsa Hassan, Tumaini Ndossi, Hawa Athumani (Vijana Queens), Judith Nyari, Hellen Simon, Shadya Amir, Kelta Kassim na Jesca Ngisaise (JKT Stars).
Wengine ni Monalisa Kaijage, Witness Mapunda, Ana Marie (Jeshi Stars), Winfrida Chikawe na Jacqueline Masinde (Polisi), Gloria Manda (DB Lioness) na Amina Kaswa (Tausi Royals).
Akizungumzia kuhusiana na kituo hicho, mmoja wa makocha anayefundisha katika kituo hicho, Denis Lipiki, anasema yeye na mwenzake Benjamin Ngogo, walipata wazo kuanzisha kituo hicho kwa lengo la kuinua mchezo huo.