CHAMA cha Mpira wa Kikapu, Mkoa wa Pwani kimepokea vifaa vya michezo kwa ajili ya ligi ya mkoa huo kutoka kwa mdau Charles Mwamwaja.
Makabidhiano ya vifaa hivyo ni mipira na pampu yalifanyika katika Uwanja wa Tumbi na kushuhudiwa na viongozi wa Serikali za mitaa kata ya Tumbi.
Baada ya kutoa mipira hiyo, Mwamwaja aliahidi kuongeza hamasa kwaa kutoa mipira kwa timu zinazoshiriki ligi hiyo kutoka Wilaya ya Bagamoyo na Kibiti na kuushauri uongozi wa chama hicho kuwa na mikakati mizuri na kuendesha mchezo huo kitaalamu.
Timu zitakazoshiriki ligi hiyo ni, Kibaha Centipedes Basketball Club, Tumbi Survivors Basketball Club, Termites Kings Basketball Club na Bagamoyo Sanaa Basketball Club.
Nyingine ni Kibiti Warriors Basketball Club na upande wanawake ni Termites Queens Basketball Club na Kibaha Centipedes Queens Basketball Club.