
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 22,2024
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 22,2024 About the author
Home » PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 22,2024 About the author
Makamu wa Rais Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhiwa tuzo kwa niaba ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa na Uhuru wa kuabudu ikiwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kupokea tuzo hiyo Katika Kongamano la Nne la Uhuru wa Kidini la Afrika leo tarehe…
*Ni sehemu ya mpango endelevu wa kusaidia jamii kwa kuchangia uboreshaji wa sekta ya Afya. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu (katikati) akipokea Vyandarua 337 na Mashuka 350 kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi mkoani humo kutoka kwa Meneja wa Benki ya Stanbic Tanzania tawi la Moshi, Hoboka Mwamakunge (kushoto )….
HISTORIA imeandikwa tena. Baada ya usiku wa jana Yanga kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya pili mfululizo ikiing’oa CBE SA ya Ethiopia, huku Clatous Chama akiendelea kung’ara katika michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Yanga ikicheza kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, ilipata ushindi wa mabao 6-0 na…
NA FAUZIA MUSSA WAZAZI na walezi wametakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa kuwalinda watoto wao na vitendo vya udhalilishaji ambavyo bado vinaonekana kuwepo nchini. Mbunge wa Jimbo la Chaani, Juma Usonge Hamadi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na walimu, wazazi na wanafunzi wa madrasat Nuru-l-huda wakati wa ufunguzi wa madrasa hiyo uiyoambatana na kusherehekea mazazi ya…
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi,akizungumza wakati wa kongamano la Binti mwenye Ndoto, lililolenga kupinga ukatili, mauaji ya watoto, wanawake na unyanyapaa dhidi ya Watu wenye Ualbino kuelekea kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani linalofanyika leo Septemba 21,2024 jijini Dodoma….
NA FAUZIA MUSSA Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kuzifariji familia 98 zilizoathiriwa na upepo mkali uliovuma katika kijiji cha Tumbatu siku za karibuni. Kufuatia tukio hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi wa Agosti, Taasisi ya Sister Island imekabidhi kilo 1350 za mchele kwa wananchi hao. Akizungumza mara baada ya kukabidhi chakula hicho, huko Kichanagani…
-Asisitiza Amani, Uvumilive na Kuheshimiana Miongoni mwa Watanzania -Serikali Yaipongeza JMAT kwa Kuhimiza Amani Nchini -Ahimiza Uchaguzi Kuunganisha Watanzania Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kulinda na kudumisha amani iliyopo nchini kwa kuzingatia misingi ya upendo, uvumilivu na…
Unguja. Wakati Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (Zipa) ikisajili miradi mipya ya uwekezaji 353 yenye thamani ya Dola za 5.5 bilioni za Marekani (Sh14.99 trilioni), uwepo wa amani na kuimarika kwa miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii vinatajwa kuvutia mitaji mikubwa ya uwekezaji kutoka nje. Miradi hiyo iliyosajiliwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya…
Na. Vero Iganatus Mkuu Wa Wilaya Ya Karatu Mhe. Dadi Kolimba awataka wanchi wa wilaya ya Karatu kutokeza kujiandikisha katika daftari la wakazi la wapiga kura zoezi ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 11/10/2024 hadi tarehe 20/10/2024. Mhe.Kolimba amesema zoezi hilo ni muhimu sana kwa wakazi wa wilaya ya Karatu kwani litawapa fursa ya kuwachagua viongozi…