Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amewapongeza wanafunzi walioshinda katika mashindano ya wanasayansi vijana marufu Young Scientists Tanzania (YST) kwani yanasaidia kupata teknolojia ambazo zitatumika kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa   utoaji wa tuzo kwa washindi wa YST Profesa Mkumbo amesema kupitia mashindano hayo vijana wamekuwa wanatafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili Jamii katika maisha ya kila siku.
“Kupitia mashindano haya  YST inaangalia kutafuta ufumbuzi wa kuangalia namna ya kutafuta  suluhisho kuhusu teknolojia kwa maisha ya baadae,”amesema Profesa Mkumbo.
Pia amesema hata tuzo ya YST Mwaka 2024 ni matokeo ya maendeleo ya utafiti  ya wanafunzi wa sekondari nchini kwa kuweka mawazo ya umakini wa kujituma katika Uhandisi wa teknolojia ya Sayansi na Hesabu nje  ya  maisha ya  darasani.
Hata hivyo amesema Taasisi ya YST imeweka mikakati kuisaidia Serikali  Kwa shule za Sekondari katika Sayansi ya Uhandisi wa Teknolojia pamoja na hesabu.