Rais Samia achangia Millioni 100 kwaajili ya ukarabati wa bwalo la shule ya msingi ya Chief zulu

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amechangia Millioni 100 kwaajili ya ukarabati wa bwalo la shule ya msingi ya Chief zulu na kuiagiza ofisi ya Halmashauri kuongezea Millioni Mia moja nyingine na kufikia lengo la Millioni 200

Hayo yamefanyika leo alipotembelea na kuzindua shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Chief Zulu iliyopo Mkoani Ruvuma

Hatahivyo Shule hiyo ya msingi Chief Zulu Academy imejengwa katika kata ya Mshangano mjini Songea kwa gharama ya shilingi milioni 500.