
September 2024


Nani awatetee wachezaji wa Tanzania!
Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Hispania, Rodrigo Hernández Cascante maarufu zaidi kama Rodri, amegonga vichwa vya habari baada ya kauli yake ya kishujaa kwa mamlaka za mpira duniani. Akiwasilisha hisia za wachezaji wengi kama siyo wote wa Ulaya, Rodri amelalamikia utitiri wa mechi unaotokana na kupanuliwa kwa mashindano. “Nadhani wachezaji tunakaribia…

BILIONI 14.5 KUSAMBAZA UMEME KATIKA VITONGOJI 135 RUVUMA KAYA 4,455 KUNUFAIKA
Mhandisi Msimamizi wa Miradi ya Umeme REA Kanda ya Kusini, Mhandisi Deogratius Nagu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme Mkoani Ruvuma kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Ahmed Septemba 30, 2024 wakati wa kumtambulisha Mkandarasi Kampuni ya CCC Intrnational Nigeria Ltd (hayupo pichani) anayetekeleza mradi wa kusambaza umeme vitongojini mkoani humo….

Kuelekea uchaguzi: Takukuru Mbeya kuvikutanisha vyama vya siasa, wagombea
Mbeya. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Mbeya imesema inatarajia kukutana na vyama vyote vya siasa mkoani humo kuwakumbusha kuzingatia kanuni za uchaguzi, hasa kuepuka viashiria vya rushwa. Uchaguzi wa serikali za mitaa umepangwa kufanyika Novemba 27, 2024 ili kupata viongozi wa ngazi za mitaa, vitongoji na vijiji kabla ya uchaguzi…

Waziri Lukuvi, atoa mitungi ya gesi kwa vijana
Waziri Lukuvi, atoa mitungi ya gesi kwa vijana Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani ameendelea kuunga mkono kampeni ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa majiko ya gesi kwa timu mbalimbali zinazoshiriki ligi ya kata ya mpira wa miguu katika jimbo la Isimani….

MATAMPI: Huyu Camara amekuja kuongeza vita
Msimu wa 2023/24, aliwaacha mbali Djigui Diarra ‘Yanga’ na Mohamed Mustapha ‘Azam FC’ akitwaa tuzo ya kipa bora si mwingine ni Ley Matampi ambaye amesisitiza kuwa na msimu huu pia anaitaka. Kipa huyo tayari ameruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye kila mchezo kati ya mechi sita walizocheza lakini amesema hilo halimpi taabu kwani kwake ni bora…

UBORESHAJI DAFTRAI LA WAPIGA KURA ZANZIBAR KUFANYIKA OKTOBA
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi katika kisiwa cha Unguja, Zanzibar leo Septemba 30, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa…

Kitabu cha maisha ya JK chaanza kuandikwa
MTENDAJI Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Institute, Kadari Singo, amesema wameanza mchakato wa kuandika vitabu viwili, cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na aliyekuwa Waziri Mkuu, Rashid Kawawa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipokuwa akitoa salamu kwenye hafla ya uzinduzi wa…

Tantrade yateuliwa kuwania tuzo za WTPO 2024
Dar es Salaam. Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeorodheshwa kuwania Tuzo za Shirika la Kukuza Biashara Duniani (WTPO) mwaka 2024 kati ya mashirika manane ya kitaifa ya kukuza biashara yaliyoteuliwa kuwania tuzo hiyo mwaka huu na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC). Tuzo za WTPO 2024 zinaangazia utendaji kazi bora wa mashirika ya…

Gamondi, Fadlu wanavyoleta mfumo mpya Bongo
Katika ulimwengu wa soka, mbinu za uchezaji zinaendelea kubadilika na kujiimarisha. Makocha wa Yanga na Simba, Miguel Gamondi na Fadlu Davids, wamefanikiwa kuingia katika anga za mbinu zinazotumiwa na makocha wakubwa duniani na kuleta staili hiyo Bongo. Wamejikita katika kutumia mianya iliyopo kati ya mabeki na kati na wa pembeni, maarufu kama “half-spaces.” Huu ni…