
Dereva, kondakta na abiria mbaroni wakidaiwa kumpiga trafiki
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 18 wakiwamo abiria 16, dereva na kondakta kwa tuhuma za kumpiga askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda. Tukio hilo limetokea juzi Jumatano Septemba 18, 2024, saa 12 jioni. Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo amesema askari huyo alikumbwa na kipigo wakati…